Andy Murray ashinda kombe la ATP ka kumshinda Novak Djokovic

Barclays ATP tennis 02 Arena. 19/11/16: Picture; Kevin Quigley/Daily Mail Andy Murray v Novak Djokovic Andy Murray wins and is world number 1Mcheza tenis kutoka Uingereza Andy Murray amemshinda mpinzani wake Novak Djokovic na kufanikiwa kushinda tuzo ya kwanza ya fainali za Dunia za ATP 2016 akiwa kama mchezaji namba moja duniani.Murray ameshinda fainali hizo kwa 6-3 6-4 katika uwanja wa O2 arena mjini London.“Nina furaha kubwa sana kuwa mshindi, na kuwa namba moja duniani ni kitu cha kipekee sana”. Alisema Murray.
Akiongeza kuwa ni nafasi ya kipekee sana kushindana na Novak katika mashindano kama haya.
Murray, mwenye miaka 29, amekuwa mchezaji bora katika mashindano 24.
Mashindano hayo pia yalimalizika kwa ushindi wa miaka minne wa Djokovic katika kinyan’ganyiro na Msebia huyo huku akimkaribia Roger Federer’s.
Murray aliyeshinda vikombe 34 kwa mara kumi ameongeza ” kabla ya hapa tumekuwa tukichuana katika fainali mbalimbali na katika Olimpiki lakini ninayo furaha kubwa kuwa mshindi.

Comments

Popular Posts