White House yakanusha madai ya Trump ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu Marekani

Image result for trumpIkulu ya White House imesema hakuna ushahidi wowote wa kuashiria kwamba kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi mkuu wa Marekani uliofanyika tarehe 8 Novemba.
Afisa wa habari wa ikulu Josh Earnest amepuuzilia mbali madai ya rais huyo mteule kwamba mamilioni ya watu ambao hawakufaa kupiga kura walishiriki katika uchaguzi huo.
Bw Trump alikuwa pia amedai kwamba kulitokea wizi wa kura katika majimbo ya Virginia, New Hampshire na California, majimbo ambayo Hillary Clinton alishinda.
“Ninachosema ni ukweli mtupu, kwamba hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai kama hayo,” Bw Earnest aliambia wanahabari White House.
Bw Trump, aliyeshinda uchaguzi kwa kupata kura nyingi za wajumbe, alikuwa amelalamika kuhusu uchaguzi huo kupitia Twitter Jumapili.
“Licha ya kushinda Kura za Wajumbe pakubwa, pia nilishinda kura za kawaida ukiondoa kura za watu ambao hawakufaa kupiga kura lakini walipiga.”
Kwenye ujumbe wa kufuatiliza, aliandika: “Ingekuwa rahisi zaidi kwangu kushinda kura za kawaida kuliko Kura za Wajumbe kwa sababu ningehitajika kufanya kampeni katika majimbo 3 au 4 badala ya majimbo 15 ambayo nilitembelea.
“Ningeshinda kwa urahisi hata zaidi na kwa njia ya kuridhisha (lakini majimbo madogo yanasahaulika)!”
Rais huyo mteule alianza kulalamika baada ya maafisa wa kampeni wa Clinton kusema wataunga mkono mchakato wa kuhesabiwa upya kwa kura katika jimbo la Wisconsin ambao ulianzishwa na mgombea wa chama cha Green Party Jill Stein.
Bi Stein pia ameifahamisha bodi ya uchaguzi katika jimbo la Michigan, ambapo ushindi wa Bw Trump wa kura 16 za wajumbe ulithibitishwa Jumatatu, kwamba ataomba kura za urais zihesabiwe upya.

Comments

Popular Posts