Mbwana Samatta ametajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika
Nahodha wa Tafa Stars, Mbwana Samatta ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji 30 wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora Afrika na Shirikisho la CAF. Mshindi wa tuzo hizi ataamuliwa na makocha wa wakuu wanaotambulika na CAF, wajumbe wa kamati ya ufundi na maendeleo ya CAF pia jopo la wataalam kwenye media. Sherehe za kutoa tuzo hizo zitafanyika Alhamis ya tarehe 4 mwezi wa kwanza 2018 huko Accra Ghana. Kampuni nguli ya nishati Naigeria ya Aiteo ndiyo itafadhili mashindano haya ya kumpata mchezaji aliyeonyesha uwezo wa hali ya juu kisoka barani Afrika.
Comments
Post a Comment