Clement Sanga athibitisha Mzambia George Lwandamina ndiye kocha mpya
Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga amethibitisha kuwa Mzambia George Lwandamina ndiye kocha mpya wa timu hiyo akichukua mikoba ya Mholanzi,Hans Van Pluijm.
Lwandamina,53,ambaye alikuwa ni kocha wa Zesco United ya Zambia, ataanza kukinoa rasmi kikosi hicho cha jangwani katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara.
Comments
Post a Comment