Hector Bellerin kuendelea kubakia Jijini London

Beki wa kulia kutoka nchini Hispania Hector Bellerin ambaye anachezea klabu ya Arsenal
amesaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki jijini London.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ameripotiwa kusaini mkataba wa muda mrefu, jambo ambalo linachukuliwa kama sehemu ya kuendeleza uwajibikaji wake, kwa kucheza katika kikosi cha kwanza cha The Gunners.
3a9f61db00000578-3957088-image-m-25_1479739766518

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger, amewathibitishia waandishi wa habari majuma kadhaa yaliyopita, kuhusu uhakika wa beki huyo kusalia katika himaya ya yake, kutokana na tetesi zilizokua zimechukua nafasi kubwa mitandaoni kuhusu mustakabali wa Bellerin.
Bellerin alisajiliwa na Arsenal mwaka 2011 akiwa kama ni sehemu ya makubaliano ya kuuzwa kwa kiungo Cesc Fabregas aliyekwenda FC Barcelona kwa wakati huo.

Comments

Popular Posts