Mke wa Donald Trump hataishi Ikulu ya White House mpaka June 2017
Mke wa Rais mteule wa Marekani Donald Trump, Melania Trump hataishi Ikulu kwasababu ya mtoto wao mwenye umri wa miaka 10, Barron Trump ambaye yuko shule kwenye mji wa New York na itakuwa ngumu kumuhamisha mpaka atakapomaliza masomo yake.
Kituo cha habari cha TMZ walinukuu maneno ya Trump alieeleza juu ya taarifa hii
“Melania hataki kusumbua maisha ya mtoto wakati bado hajamaliza shule yake, kwahiyo bado wataishi kwenye jumba la Trump Tower jijini New York mpaka June 2017 ndipo watahamia Ikulu, kwasasa hawezi kumuweka mtoto wake mbali na marafiki zake, michezo na shule yake, atakapomaliza June watahamia Washington D.C’ – Donald Trump
Trump alisema Melania atakuwa akienda Ikulu akimuhitaji na kurudi nyumbani mjini NYClakini mtoto hatahangaishwa mpaka amalize shule mwanzoni mwa June 2017 na hakuna kitakachobadilishwa kwenye kauli hii kwani wameshaamua hivyo kama familia.

Melania akiwa na mtoto wake Barron
Comments
Post a Comment