Schweinsteger ashinda tuzo ya heshima Ujerumani

15034631_1759012674337766_1085051151495200768_n
Kiungo wa timu ya Manchester United, Bastian Schweinsteiger amefanikiwa kushinda tuzo ya heshima ya Special Jury kutokana na mchango wake aliowahi kuutoa kwenye timu yake ya taifa ya Ujerumani.
Naye kocha wa timu hiyo ya taifa, Joachim Low alifanikiwa kushinda tuzo hizo zinazoandaliwa na vyombo vya habari vya nchini humo ambazo hujulikana kwa jina la Bambi Awards.
Mchezaji huyo ambaye alikuwa kepteni wa timu hiyo ya taifa ya Ujerumani alitangaza kustaafu kuichezea timu hiyo mwezi Agosti mwaka huu lakini ameonekana kuwa na msimu mbaya chini ya kocha Jose Mourinho alipowasili klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu

Comments

Popular Posts