Sir Elton John aikataa ofa ya Donald Trump
Awali mmoja ya Kiongozi wa karibu wa Trump, Anthony Scaramucci aliiambia BBC kuwa mwanamuziki huyo wa Uingereza atatumbuiza kwenye sherehe hizo zitakazofanyika Januari 20, mwakani.
“Elton John is going to be doing our concert on the Mall for the inauguration,” alisema Scaramucci. Imedaiwa kuwa Elton alikuwa akimuunga mkono Hillary Clinton tangu alipokuwa akitumbuiza kwenye hafla ya mgombea huyo ya uchangishaji wa pesa iliyofanyika mjini Los Angeles mwezi uliopita.
Hata hivyo imedaiwa kuwa sababu nyingine iliyochangia mwanamuziki huyo kukataa ofa ya Trump ni hutokana na Rais huyo mteule kutumia wimbo wake wa Rocket Man and Tiny Dance bila idhini yake kwenye kampeni zake za urais.
Comments
Post a Comment