Wafuasi wa Clinton wataka kura katika majimbo 3 muhimu zihesabiwe upya kwa mkono

Image result for Hillary ClintonHillary Clinton anaongoza kwa kura milioni 2 alizopigiwa na wananchi (popular votes) dhidi ya Rais mteule wa Marekani, Donald Trump.
Kwa mujibu Cook Political Report, Hillary ana kura milioni 64.2 dhidi ya milioni 62.2 za Trump. Ni mara ya tano sasa mshindi wa kura za nyingi za wanachi anashindwa uchaguzi.
Na sasa wafuasi wa Clinton wanamtaka ayapinge matokeo ya majimbo ya Michigan, Pennsylvania na Wisconsin. Wamepata ripoti kutoka kwa mtaalaam wa computer anayedai kuwa matokeo ya Michigan, Pennsylvania na Wisconsin, yaliyompiga ushindi Trump wa Electoral College, yanahitajika kupitiwa tena kwa mkono kuhakikisha kuwa hakukuwa na wizi.
Hata hivyo pendekezo hilo limeonesha kutoiingia akilini mwa kampeni ya Clinton ambayo inaamini kuwa zoezi hilo litakalotumia gharama kubwa na muda mwingi, halitobadilisha kitu.

Comments

Popular Posts