Mabadiriko katika baraza la mawaziri yaliyofanyika leo na Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya mabadiriko katika baraza lake la mawaziri ambapo baadhi ya mawaziri wamepoteza nafasizao huku baadhi ya wengine wakipanda  huku wengine wapya wakiteuliwa miongoni mwao naibu wa nishaati amepanda cheo na kuwa waziri

Mabadiliko ya hayo yaliyofanyika yamefanya kuongezwa kwa wizara mbili, hivyo kufikia wizara 21 kutoka 19 ambazo zilikuwepo.

Tukio hilo limetokea leo ambapo Rais Magufuli pia amezigawa Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na kuwa wizara ya Kilimo pekee na Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake, pamoja na Wizara ya Nishati na Madini kuwa wizara mbili tofauti.

Sambamba na hilo pia Rais Magufuli amemteua Mh. George Haruna Mkuchika kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora, ambaye kabla alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mawaziri hao wanatarajiwa kuapishwa siku ya jumatatu Oktoba 9, 2017, Ikulu jijini Dar es salaam. 

Comments

Popular Posts