Raisi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Ametembelea Kiwanda cha Bidhaa za Urembo


Raisi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametembelea kiwanda ya bidhaa za urembo mjini Pyongyan akiandamana na mke wake Ri Sol-ju na dada yake Kim Yo-jing.

Kuoneka hadharani kwa Kim Yo-jong, kunakuja muda mfupi baada ya kupandishwa cheo ndani serikali ya Korea Kaskazini.
Bidhaa za urembo kutoka nchi za kigeni zimekuwa adimu nchini Korea Kaskani kutokana na vikwazo.

Korea Kaskazini inaonekana kujenga sekta yake ya bidhaa za urembo ambapo bidhaa kama Bomhyanggi na Unhasu vimepata umaarufu.
Licha ya umaarufu wake wa kupigwa picha akiwa katika vituo vya kijeshi na maeneo ya kufanyia majiribio makombora, ziara ya Kim katika kiwanda cha bidhaa za urembo ni moja ya propaganda ya kuhalalisha utawake wake kwa watu wa Korea Kaskazini.

Ziara hiyo "ni ya kuonyesha kuwa Korea Kaskazini inaweza kuwatunza watu wake na kuleta maendeleo kwa kiwango sawa na cha China na Korea Kusini," mdadisi wa masuala ya Korea Kaskazini Ankit Panda aliiambia BBC.
"Licha ya sisi kujua kuwa sio ukweli, ni muhimu kwa utawaka huo kuonyesha watu wake kuwa unaweza kuwapa bidhaa wanazozihitaji,"

Wakati wa ziara hiyo , Kim alikisifu kiwanda hicho kwa kuzalisha bidha za kiwango cha kimataifa, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la KCNA.

Comments

Popular Posts