Alikiba adaiwa kumtupia dongo Diamond baada ya kuandika amewaona ‘Simba Original’

zzzzaaJumanne hii ilikuwa ni birthday ya mkali wa wimbo Aje, Alikiba ambapo aliungana na uongozi wake kwenda mbuga ya wanyama ya Serengeti National Park kwa ajili ya kusherekea siku hiyo muhimu katika maisha yake.

Hata hivyo mkali huyo amechafua hali ya hewa mitandaoni baada ya kuposti picha yake wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na kuandika maneno kuwa anawaangalia Simba Original ambapo ujumbe huo umetafsiriwa kama kijembe kwa staa mwenzake Diamond Platnumz ambaye naye ujiita Simba.

Comments