Kenya yampa ubalozi Jaguar
NYOTA ya muziki wa Kenya, Charles Njagua (Jaguar), imezidi kung’aa baada ya kuzidi kujiongezea wigo mpana wa kuaminika mara baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa maji nchini humo.
Naibu Rais nchini humo, William Ruto pamoja na Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Eugene Wamalwa, walimkabidhi tuzo ya ubalozi msanii huyo juzi mjini Nairobi, kwenye ukumbi wa KICC.
Licha ya kuwa balozi wa maji, msanii huyo pia ni balozi wa kupinga dawa za kulevya kupitia shirika la NACADA.
“Ninajisikia kuwa na furaha kubwa kwa Waziri wa Maji kunichagua kuwa balozi katika idara yake, ninaamini nitakuwa balozi wa kweli,” aliandika Jaguar.
Comments
Post a Comment