Kipa Mghana wa Simba awasili Tanzania
Kipa Daniel Agyei ametua nchini leo saa saba akitokea nchini Ghana kwaajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuchezea Simba.
Agyei aliyekuwa akiichezea Medeama,amewasili kwa ndege ya shirika la KQ na kupokelewa na mratibu wa timu ya Simba,Abbas Ally.
Baada ya kutua kipa huyo amepelekwa kwenye hoteli ya Sapphire jijini kabla ya kukutana na uongozi wa Simba kwa ajili ya kusaini mkataba huo.
''kwa sasa amekwenda kupumzika na leo jioni au kesho ndipo atakutana na uiongozi kwa ajili ya kukamilisha usajili wake''anasema Abbas
Comments
Post a Comment