Ndege iliyobeba wachezaji wa Brazil yaanguka Colombia
Ndege iliyokuwa imebeba watu 72, ikiwemo timu ya soka ya klabu ya Chapecoense ya Brazil, imeanguka katika sehemu ya milima nchini Colombia wakati inakaribia Mji wa Medellin.
Maelezo kamili ya ajali hiyo hayajafahamika lakini habari zinasema kwamba kuna watu 6 walionusurika.
Ndege hiyo ya kukodisha iliyokuwa ikitokea Bolivia, ilikuwa na timu ya soka ambayo ilikuwa icheze katika fainali ya Kombe la Amerika ya Kusini dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya Medellin. Hivyo, fainali hiyo imeahirishwa.
Ripoti zinasema ndege hiyo yenye leseni namba CP 2933, iliyoanguka muda mfupi kabla ya saa sita usiku, ilielezewa na Meya wa Medellin, Federico Gutierrez, kama “janga kubwa”, akiongeza kwamba inawezekana kuna watu walionusurika.
Comments
Post a Comment