Rosberg atwaa ubingwa wa Formular 1 2016

3acdf38e00000578-3975950-image-a-2_1480272671554Mjerumani Nico Rosberg amefanikiwa kuchukua ubingwa wa Formular 1 baada ya jana usiku kumaliza wapili katika mbio za Abu Dhabi Grand Prix ambapo mpinzani wake kutoka timu moja ya Mercedes, Lewis Hamilton akimaliza wa kwanza na namba 3 akishika Sebastian Vettel wa Ferrari.

Nico Rosberg amechukua ubingwa huo wa 2016 kwa tofauti ya pointi 5 na Lewis, Nico amemaliza akiwa na pointi 385, huku Hamilton akifikisha 380 na namba 3 ikikamatwa na Daniel Ricciardo wa Red Bull mwenye pointi 256.

Comments