UFAFANUZI Kuhusu kauli ya Waziri Ndalichako kwa wanaojiunga Vyuo Vikuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zilizoenea ya kuwa, Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako amezuia wanafunzi wenye Stashahada (Diploma) kujiunga na masomo ya Shahada (Degree) katika vyuo vikuu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa, katazo lililotolewa na Waziri Prof. Ndalichako siku ya mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania linawahusi wale tu wanaosoma Foundation Courses ili kuweza kujipatia sifa za kujiunga na chuo kikuu.
Taarifa imeeleza kuwa awali wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne walikuwa wakisoma Foundation Courses katika vyuo mbalimbali na kisha kujipatia sifa za kujiunga na chuo kikuu kitu ambacho waziri alisema sasa hakitakuwepo tena.
Utaratibu huu ulikuwa ukitumika zaidi katika Chuo Kikuu Huria ambapo wanafunzi walikuwa wakisoma programu maalum zilizokuwa zikiwapa sifa ya kusoma Shahada.
“Kilichojitokeza ni kuna taarifa zinasambaa kwamba kuanzia sasa wanafunzi watakaoenda chuo kikuu ni wale ambao tu wamepitia form six sasa hiyo taarifa imeleta presha kubwa, nimekuja hapa sio kukataa tamko hilo hapana nimekuja kulitolea ufafanuzi.” – Naibu Waziri Eng. Stella Manyanya
Comments
Post a Comment