Roma, Moni na wenzao 2 waachiwa rasmi, Jumatatu kueleza A-Z kuhusu tukio zima
Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wenzao 2 wameachiwa na jeshi la polisi baada ya kuhojiwa na kufanyiwa vipimo.
Wasanii hao walitekwa na watu wasiojulikana Alhamisi hii wakiwa Tongwe Record na mapema Jumamosi hii walionekana wakiwa oysterbay polisi.
Akiongea na waandishi wa habari akiwa Mwananyamala hospitali muda mchache baada ya kufanyiwa vipimo na kuachiwa huru, Roma alisema kwa sasa anaendelea vizuri pamoja na wenzake.
“Kutokana na mazingira na situation nzima hatutakuwa na muda mrefu zaidi wa kuongea zaidi ya dakika moja. Lakini niwahakikishie mimi ni mzima mpaka sasa hivi, niko njema kabisa, kiafya, kiakili na kivingine. Hata wenzangu watatu nikimaanisha, Moni, Bin Laden pamoja na Imma wote ni wazima,” alisema Roma.
Aliongeza, Tuko katika taratibu za kutoa taarifa za tukio zima ambalo limetokea, taratibu hizo zinatufunga kwa sasa tushindwe kuzungumza. Lakini ratiba ambayo naweza kuwapatia Jumatatu nadhani tutakuwa na press conference kueleza nini kilitokea,”
Comments
Post a Comment