VIDEO: Juventus VS FC Barcelona robo fainali ya UCL

Baada ya mapumziko mafupi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa April 11 2017 mchezo wa kwanza wa robo fainali kati ya Juventus dhidi ya FC Barcelona ulichezwa mjini Turin wakati mchezo wa Borussia Dortmund dhidi ya Monaco ukiahirishwa hadi April 12 saa 19:45 EAT kwa sababu za kiusalama.
Mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Juventus nchini Italia ulianza kuibeba Juventus kuwa na rekodi ya kutowahi kufungwa na Barcelona katika ardhi ya Italia, wakiwa wamewahi kutoka sare mara mbili na Barcelona kupoteza mara mbili wakati mara ya mwisho kukutana ilikuwa Berlin katika mchezo wa fainali UEFA Champions League 2015 na Juventus akapoteza kwa magoli 3-1.

Juventus wakiwa Turin katika mji wao na sapoti kubwa ya mashabikiwa wao wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0, magoli yakifungwa na Paulo Dybala dakika ya 7 na 22 na goli la mwisho likafungwa na Giorgio Chiellini dakika ya 55, Juventus na Barcelona watacheza mchezo wa marudiano April 19 Nou Camp.

Comments